... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Matunda Yapasayo Toba

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 3:8 Basi zaeni matunda yapasayo toba.

Listen to the radio broadcast of

Matunda Yapasayo Toba


Download audio file

Je!  Umewahi kujaribu kuachana na tabia yako mbaya?  Sio rahisi.  Hailishi kama ni uvutaji wa sigara, kula vibaya, umbeya au nini – kawaida mwanadamu anajitahidi kuiacha lakini hatimaye anashindwa.

Ukweli ni kwamba kujibadilisha sisi wenyewe na kuwa na mwelekeo mpya unaotakiwa, njia tunaoijua kuwa sahihi, kunakuwa vigumu sana.

Zamani, Yohana Mbatizaji alikuwa anaandaa taifa la Israeli kwa ajili ya ujio wa Yesu, Masihi wao.  Alisema hivi:

Mathayo 3:8  Basi zaeni matunda yapasayo toba. 

Toba linaanza na mabadiliko moyoni.  Mabadiliko hayo moyoni, kwa mtazamo wa Mungu, yanatazamiwa kuleta matunda mapya, mazuri, ya kudhihirisha kupitia mienendo yetu kwamba tumemrudia Mungu.

Kama vile A.W. Tozer alivyosema, Tusipobadilishwa na neema ya Mungu, basi tutakuwa hatujaokolewa na neema yake.

Kama ningekwambia kwamba nilijibadilishia maisha yangu mimi mwenyewe, kwamba nilishinda mapepo mabaya yote, kwamba kwa kupitia matendo yangu mema nikageuka kuwa mtu mwema.  Lakini ningekuwa mwongo kabisa.  Uwezo wa kubadilika unatokana na jinsi mtu anamfungulia Mungu moyo wake na kuanza kuelewa na kupokea neema yake ya ajabu, kupitia sadaka ya Yesu pale Msalabani wakati alilipa hukumu ya dhambi zake aliyostahili kuipokea.

Kubadilika, lazima tubadilike.  Basi zaeni matunda yapasayo toba.   

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.