... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Msingi wa Utakaso

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wathesalonike 4:3-6 Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukana na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu. Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana.

Listen to the radio broadcast of

Msingi wa Utakaso

Download audio file

Kujitakasa, hajilishi ni jambo gani katika maisha yako, ni vigumu.  Yaani tabia za zamani ni vigumu kuzivunja na kuziacha.  Tabia zile zinanang’ania sana zikitaka kutuangusha kila wakati. Au labda ni mimi peke yangu!?

Zoezi la kujitakasa wanatheolojia wanaliita “utakaso”.  Sasa kutokana na upendo mkubwa wa Mungu; …Mungu anatuita kwenye utakaso:

1 Wathesalonike 4:3-6  Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukana na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.  Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana.

Kumbe, ni onyo kali kabisa; onyo linalolenga moja kwa moja mwelekeo wetu wa kuhesabu dhambi zetu kuwa si kitu kabla ya kuzificha.

Usidanganyike – Mungu aliona uzito wa dhambi zetu kuwa ni kubwa kiasi cha kumtuma Yesu kufa msalabani ili alipe adhabu iliyodaiwa na haki yake.  Umwamini yeye na dhambi zako zote zitasamehewa kabisa.

Mungu anakuita uishi maisha mapya.  Anataka kukuweka huru na matokeo ya dhambi zako; kwa kukutakasa.  Si kazi unayopaswa kuifanya peke yako, Amesha mtuma ROHO wake Mtakatifu ili akuwezeshe, ili akutakase.

Kwa hiyo, unapojaribiwa na kuona dhambi yako ni jambo jepesi, kumbuka kwamba, haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.

We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy