Msingi wa Utakatifu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Waebrania 12:14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao.
Acha nikuuliize leo swali la tafakari kidogo halafu unijibu. Je!, Kipaumbele kilichopo maishani mwako ni kipi? Eeh, vipaumbele ndivyo vinavyomwongoza mtu katika maisha yake.
Kama hatuchunguzi vipaumbele vyetu mara kwa mara, tutajikuta tunaishi katika mazoea tu bila kufikiria, na ni ajabu kuona namna maisha yanavyokwenda kasi.
Kipaumbele changu cha kwanza ni kumheshimu Mungu. Kila asubuhi natafakari hilo na kuliombea. Bado inanishangaza mno jinsi Yesu alivyokufa kwa ajili ya dhambi zangu. Kwahiyo; ninampenda, ninataka kumheshimu na ninataka kumwishia. Ndivyo nilivyo mimi. Wewe, je! Ni kipi kinachotanguliza orodha ya vipaumbele vyako?
Kama tulivyoona siku chache zilizopita, ni baraka kubwa kujua kwamba hatuhitaji kujaribu kutimiza lengo hilo kwa kutumia nguvu zetu. Mtu akimwamini Yesu, Mungu anampa Roho yake, Roho Mtakatifu, ili amsaidie kusafisha mwenendo wake kama vile wanatheolojia wanavyosema, “kumtakasa”…kumfanya awe mtakatifu.
Lakini; na sisi tuna sehemu katika zoezi hili; ni kumheshimu Mungu; na kufanya ule “utakatifu” kuwa kipaumbele chetu cha kwanza kabisa. Huu ndio utofauti kati ya mwamini na mwanafunzi; kati ya mtu anakubali kwa kichwa kwamba Yesu alikufa kwa ajili yake.. na yule anayemwishia yeye kwa moyo wake wote.
Waebrania 12:14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao.
Ina maana, weka utakatifu kuwa kipaumbele maishani mwako; weka kumheshimu Mungu kuwa kipaumbele maishani mwako; weka kuishi na kutembea na hata kuvuta pumzi kwa ajili yake – kuwa kipaumbele chako cha kwanza.
Utakatifu – utakatifu wako – ni ushirikiano. Hauhitaji kuutafuta peke yako, lakini bado unahusika kwa sehemu kubwa.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.