Mtazamo Ulio Mpana
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 118:5,6 Katika shida yangu nalimwita BWANA; BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi. BWANA yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?
Kuna mapambano mengi maishani. Sasa, mtu akiwa anapambana, anataka sana ashinde. Mara nyingi si muhimu sana mtu ashinde, lakini wakati mambo yanapamba moto, anaona kwamba lazima ashinde.
Je! Unapigana mashindano leo hii? Je ni mashindano ya mahusiano, au ya uchumi, afya au swala ni linalokutafuna kwa ndani? Na unatambua kwamba ni lazima ushinde kabisa.
Nilikuwa ninamtembelea mzee mmoja hospitalini ambaye ana kansa mbaya yenye hatua za mwisho – mwanamume mwenye imani kubwa kwa Mungu. Aliniambia hivi, “Bado mimi ninajisikia kwamba ninao uzima mwingi ndani yangu. Haiwezekani nimefikia muda wangu wa kufa.”
Zaburi 118:5,6 Katika shida yangu nalimwita BWANA; BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi. BWANA yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?
Ni kweli, kuna wakati tuna shida kabisa na inabidii tumwite Mungu atusaidie. Kwa njia yake na kwa wakati wake, daima anajibu wakati watu wake wanaomwita. Lakini maisha haihusu kushinda katika mapambano ya hapa chini duniani tu, mapambano ambayo hayana umuhimu ukizingatia habari ya uzima wa milele.
Kwa sababu siku moja, kwako wewe na kwangu mimi, mapambano mengi hayatakuwa na umuhimu tena. Siku moja tutaona kwamba jambo lililo muhimu peke yake ni jinsi tulivyoweza kuishi tukimtegemea Yesu.
Haijalishi unakabiliana na shida gani, hata swala la kuishi au kufa, ujue kwamba Mungu yu pamoja nawe, kwa hiyo usiogope. Hakuna awezaye hapa duniani kukunyanganya yale yote aliyoandaa kwa ajili yako. Huu ndio mtazamo mpana sana.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.