... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mtego wa Utajiri

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Kumbukumbu 8:17,18 Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo. Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri.

Listen to the radio broadcast of

Mtego wa Utajiri


Download audio file

Je!  Inaeleweka au haieleweki mtu ambaye anakiri kuwa Mkristo, kuwa na akiba kwa ajili ya kustafu wakati bado kuna watu duniani ambao wanakufa na njaa na hata karibu yake, kuna watoto wanaishi mitaani?

Ni swali linaloweza kuchanganya kwa sababu ya utofauti mkubwa wa hali ya uchumi na mazingira mbali mbali ya watu wanaoishi duniani – hata kati ya watu wanaosikiliza kipindi hiki kwenye redio – yaani wote hawalingani kabisa.

Ninakumbuka mwalimu mmoja aliyetufundisha wakati nilikuwa ninasoma chuo cha Biblia zamani, jinsi alivyosema, Kama haiwezi kumfaidia tajiri na maskini pia, mweusi na mzungu … basi si Injili.  Na mimi ninakubaliana naye.  Sasa swali lililopo ni hili, je!  Matajiri, inawapasa watumieje mali waliyo nayo?  

Kwa upande mmoja,  Yesu alitufundisha kutokujiwekea hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali kujiwekea hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi.

Lakini kwa upande mwingine, ni jambo la busara kuwa na akiba angalau kwa ajili ya mahitaji yetu, hususani wakati tunaanza kuzeheka.  Biblia inazung’umza habari ya kufanya kazi kwa nguvu na kuweka akiba pia.  Lakini haijalishi ukoje kiuchumi:

Kumbukumbu 8:17,18  Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo.  Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri.

Daima, kiburi ni mtego unaotokana na mali.  Yo yote uliyo nayo, yametoka kwa Bwana.  Njia mojawapo kuepuka mtego huo na kujiwekea hazina mbinguni ni kutoa, si kutoka kwa ziada uliyo nayo, lakini kwa ukarimu kabisa.

Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo.   

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy