Mtikiso wa Neema
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Tito 2:11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa.
Wakati mtu anakuonyesha fadhili, hata katika jambo dogo, je! Inabadilishaje unavyomwona, jinsi unamtazama na kumtendea?
Bila shaka, tendo la wema lilitokana na upendo, ni kitendea kazi chenye nguvu cha kuleta mabadiliko katika ulimwengu – hususani wakati aliyefadhiliwa anafahamu vema kwamba hastahili.
Wema wa namna hio kwa mtu asiyestahili unaitwa neema.
Halafu hakuna wema mkubwa kwa wasiostahili, wema uliotoka kwa pendo kuu kuliko neema ya Mungu iliyoonekana wakati Mungu alimtuma Mwanae kufa kifo cha ukatili pale Msalabani ili alipe deni la dhambi zetu, za kwako na za kwangu, tuweze kwa kumwanini huyu Yesu kupokea karama bure ya uzima wa milele.
Sasa hayo yamekusudiwa kubadilisha jinsi tunavyomwona Mungu na kumwitikia.
Tito 2:11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa.
Ninakusihi kwa moyo wangu wote, upokee moyoni neema hii ya Mungu iliyomfanya atume Yesu kufa kwa ajili ya dhambi zako ili uweze kusamehewa. Alifufuka pia akuletee maisha mapya yatakayoendelea milele na milele.
Ruhusu wema huo usiostahili ukubadilishe, ubadilishe mwenendo wako tangu sasa, kwa sababu neema ya Mungu imekuja … kwa ajili yako.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.