Mtumishi Mwenye Moyo
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
2 Wakorintho 3:6 Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.
Pengine umeshasikia habari ya vimeng’enya, lakini je! Unakumbuka kazi yao? Vimeng’enya ni aina ya protini ndani ya mwili vinavyochochea mjibizo katikati ya kemikali mbali mbali.
Sitaki kukuingiza darasani kwenye kozi ya sayansi sekondari, hapana. Ila natoa mfano tu. Vimeng’enya vina kazi kubwa ndani ya mwili ili mtu awe na afya njema. Havihusiki moja kwa moja na mchakato wa kemikali, lakini vinasababisha mchakato huo utokee na kuufanya uende kasi.
Na ndivyo anavyofanya Roho Mtakatifu maishani mwetu. Yeye anasababisha mambo kadha yatokee hata kusababisha viende kasi, mambo mema yanayopaswa kutokea lakini yanayotushinda kuyatekeleza bila msaada wake.
2 Wakorintho 3:6 Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.
Yote anayetuagiza Mungu tuyafanye ni kwa manufaa yetu. Pia, makatazo yake (si mengi zaidi) yanaeleweka vizuri. Kwa nini sasa, tunashindwa kufanya mapenzi yake na kuacha kutenda yale aliyotukataza tusiyafanye? Hapo ndipo tunahitaji Roho Mtakatifu kutuonekania. Yeye ndiye kama kimeng’enya, kichocheo kutuelekeza kwenye utakaso, kwenye utii – anayesababisha itokee na kwenda kasi.
Ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.