... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mtuombee

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Wathesalonike 3:1,2 Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa vile vile kama ilivyo kwenu; tukaokolewe na watu wasio haki, wabaya; maana si wote walio na imani.

Listen to the radio broadcast of

Mtuombee


Download audio file

Nakupa taarifa kwamba; leo tumeandaa kipindi ncha elfu mbili mia moja na arobaini na sita cha NENO SAFI LENYE AFYA kwa ajili yako hapa kwetu kwenye studio ya Christianityworks (yaani Ukristo Unafanya Kazi). Taarifa hii labda utaona kwamba haisaidii chochote.

Kwanini sasa nimekwambia taarifa hiyo?  Si kwamba hesabu ya 2,146 imetufikisha kwenye hatua maalum wala tukio muhimu la kihistoria. 

Ni kwamba, haijalishi unaona kipindi hiki kwenye TV au unakisikiliza kwenye redio katika lugha mmojawapo au kikisoma kwenye karatasi au barua pepe au kwenye WhatsApp au tovuti yoyote ya kidijitali, bado ninajiuliza; kama umewahi kutafakari kazi yote ya kuandaa na kutengeneza kipindi kama hiki. 

Kwanza kuna kuandaa maneno na kuyaandika, halafu kutafsiri kwa lugha mbalimbali, kuhakiki tafsiri, kuyasoma na kuyarekodi audio na kushuti programu kwa ajili ya TV, kuzipeleka kwenye vituo mbalimbali, nakuziupload pamoja na picha kwenye tovuti mbalimbali na kuchora kitakachoprintiwa … yaani inachanganya, sindiyo? 

Lakini kama ilivyo kwenye shughuli yoyote yenye maana, kweli juhudi zinatakiwa ndani ya timu ndogo ya watu wanaojitolea kutimiza huduma hii.  Kwahiyo, leo nataka utupe kitu kimoja, yaani tupate fadhili zako: 

2 Wathesalonike 3:1,2  Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa vile vile kama ilivyo kwenu; tukaokolewe na watu wasio haki, wabaya; maana si wote walio na imani. 

Kadiri tunavyoendelea kuzidi kufikia watu na kuwashirikisha Neno la Mungu kupitia Neno Safi Lenye Afya, ndivyo tutavyozidi kuona mabadiliko maishani mwa watu.  Na ni kweli, kuna sehemu zingine duniani kufanya kazi hii ni hatari. 

Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa vile vile kama ilivyo kwenu; tukaokolewe na watu wasio haki, wabaya.   

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy