Muda Unaenda
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Warumi 13:10,11 Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria. Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwaidia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini.
Umebakiza muda gani ili uwapende wanaokuzunguka?, Lini itakuwa wakati wako wa mwisho wa kukumbatia mpendwa wako?….Jibu ni kwamba, hatujui. Ndio maana upendo unapaswa kuwa kipaumbele chetu.
Ni wazo linalofadhaisha, Maisha yanaweza kukatishwa ghafla, mtu akafa bila kutazamia. Siku moja nitambusu mke wangu Jacqui na kumkumbatia kwa mara ya mwisho. ghafla, mmoja wetu atakuwa ameondoka. Hii ni kweli kwa wote unaowapenda katika maisha yako.
Si wapenzi tu!. Hata watu wanaokusumbua, wakorofi. Siku moja mahusiano yako na yao yataisha, itakuwa ni msiba mkubwa
Warumi 13:10,11 Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria. Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwaidia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini.
Ni kweli, tunaishi kipindi chenye maana; wakati wa majaribu, wakati wa mapambano, wakati mpasuko unazidi kuenea kwenye jamii na hata katika mahusiano yetu na watu wengine. Kwahiyo, sikiliza sauti ya kukuamsha:
Saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia.
Wapende wale watu uliokuwa unawaumiza … Kwasababu kuwapenda ni kutimiza sheria ya Mungu. wapende. Kwasababu mwisho wa mambo yote umekaribia, umekaribia sana kuliko tulipoanza kuamini.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.