Mungu Hawezi Kusema Uongo
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Waebrania 6:18 Ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu.
Kuna jambo moja ulimwenguni ambalo tunaloweza kutegemea kabisa. Hata ikiweje, hata dhoruba ikipigaje kwa nguvu kiasi gani, tunaweza kuwa na uhakika kwamba chini ya miguu yetu kuna ardhi isiyoweza kutikiswa … ila hadi pale inaanza kutikisika kwa tetemeko la ardhi!
Je! Ni mambo gani maishani mwako unayotegemea kuwa imara kabisa; kama vile ardhi ngumu chini ya miguu yako? Je! Ni familia yako, nyumba yako, ajira yako … mambo ambayo kamwe hayawezi kukuangusha?
Lakini hata hivi, hata kama hutaki kuifikiria, moyoni kabisa unajua kwamba siku moja hayo yote yatapita.
Lakini kuna kitu kingine nakubali kwamba hakiwezi kubadilika, tena si mimi tu peke yangu. Ni uaminifu wake Mungu. Kumbuka kwamba mimi ni mhubiri! Lakini sijui kama umeshaelewa kwamba hata mtumishi wa Mungu anaweza kuwa na mashaka akibanwa na matatizo; wakati hofu inatikisa imani yake; wakati msiba ule mkubwa unazidi kumkaribia?
Kwa hiyo inatakiwa leo tujikague; inatakiwa tupewe Neno lenye nguvu, Neno la faraja:
Waebrania 6:18 Ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu.
Ndiyo maana … mimi binafsi nategemea sana Neno lake, yaani Biblia. Kwa sababu Mungu akitamka neno, ni kweli kabisa. Hawezi kusema uongo. Kwa hiyo rafiki yangu, ninakutia moyo umfanye kimbilio chako, ujifiche ndani yake na kushika tumaini lako la hakika. Kwa sababu …
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.