... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mungu Kuonekana kwa Watu Wote

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 1:18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua

Listen to the radio broadcast of

Mungu Kuonekana kwa Watu Wote


Download audio file

Kwa watu wengi, dhana ihusuyo “Mungu” inaonekana kuwa kitu ambacho hakishikiki.  Labda mtu anaweza kuwaza habari zake mara kwa mara, akaingiza hata dua fupi kwake, lakini katika pirika za maisha hakuna la ziada.  Je!  Wewe binafsi ukoje?

Shida iliyopo katika kujaribu kumjua Mungu, hata akiwa nani, ni kwamba mtu hawezi kumwona.  Hamwezi kuketi pamoja kuchangia chai au kahawa, kama rafiki yako

Hakuna aliyemwona Mungu, kwa hiyo mtu angewezaje kukabidhi maisha yake kwake?  Mtu atawezaje kuamini anachokisema?

Yohana 1:18  Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.

Je!  Hapo Mungu anataka kusema nini kupitia mmoja wa wanafunzi wake aitwaye Yohana?  Ni kwamba, anaweka wazi shida iliyopo.  Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote … Isipokuwa “Mungu Mwana pekee” … Isipokuwa Yesu peke yake.

Kwa hiyo Mungu amemtuma Yesu kufanyika kuwa mwanadamu – ni yale tuliyosherehekea siku mbili zilizopita wakati wa Krismasi – huyu Yesu, aliyemwona Mungu, aliye Mungu, aliye karibu sana na moyo wa Baba kwa kusudi la … kutufunulia Mungu.

Je!  Unataka kujua Mungu yukoje; kujua anawaza nini, kufahamu mwitiko wake, kujua kinachomsisimua, kinachomkasirisha, kujua uweza wake ulivyo pamoja na wema wake na pendo lake?  Umwangalie Yesu tu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy