Mungu ni Mwema
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 86:5 Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, umekuwa tayari kusamehe, na mwingi wa fadhili, kwa watu wote wakuitao.
Sijui kama umeshaona jinsi ilivyo rahisi kupoteza dira na kuacha kuzingatia yaliyo muhimu maishani kwa sababu ya kupambana na changamoto za kila siku? Ndiyo maana inatubidi mara kwa mara, kukumbushwa habari za mambo yaliyo muhimu zaidi.
Nina mke mwema kabisa. Jacqui ana moyo wa mtumishi. Pia ni mbunifu sana akifuma sweta kwa ajili ya familia, akipika keki kwa kusherehekea siku za kuzaliwa za wajuguu na kadhalika. Pia ananipenda sana.
Sasa mimi, ninaishi maisha yenye pirika-pirika. Usinielewe vibaya, kwa kweli ninapenda huduma yangu sana lakini inanigharimu masaa mengi tukipambana na ishu nyingi ngumu duniani kote. Kwa hiyo ni rahisi kuzubaishwa na kusahau jinsi Jacqui anavyonipenda. Na hii ni hatari.
Na ndivyo ilivyo rahisi kwetu kusahau upendo wa Mungu kwetu – upendo mkubwa kiasi cha kusababisha Yesu atoe uhai wake ili tuweze kuwa na mahusiano mema naye, mahusiano yanayoridhisha kabisa.
Kwa hiyo, kwa tahadhari kwamba yamkini leo unahitaji kukumbushwa, acha nitaje kumbukumbu niliyogusia mwanzoni:
Zaburi 86:5 Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, umekuwa tayari kusamehe, na mwingi wa fadhili, kwa watu wote wakuitao
Rafiki yangu, Mungu ni mwema, kila wakati. Haijalishi umefanya nini, daima atakusamehe kabisa – ndiyo maana Yesu alikufa kulipa deni la dhambi zako, ili uweze kusamehewa. Na pendo lake kwako linafurika kutoka moyo wake masaa 24 kila siku ya wiki kuanzia leo hadi milele daima.
Kinachohitajika kwako ni kitu kimoja tu. Ni kumwita yeye, na atakukirimia wema wake, msamaha wake, na fadhili zake endelevu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.