... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mungu wa Tumaini Tele

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Warumi 15:13 Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.

Listen to the radio broadcast of

Mungu wa Tumaini Tele


Download audio file

Je!  Umewahi kujiuliza ni mtu gani watu wanakutana naye wakati wanaonana na wewe?  Yaani wanakufikirije mkikutana?  Mtu anayechangamka au mtu aliyekatishwa tamaa?  Mtu wa furaha au mtu anayechukiza?  Mtu mwenye fadhili au mtu mwenye hila?  Sijui kama ulishajiuliza unaonekanaje mbele za watu?

Usiku, nikienda kulala, ninaanza kufikiria watu ambao nilikuwa nao mchana.  Ninaanza na mke wangu –Nilimtia moyo na kumfanya ajisikie kupendwa, au labda nilimkasirisha?  Je!  Mkutano ule tuliofanya na timu yetu India kupitia mtandao – Je!  Niliwafanya wajisikie kama wamethaminiwa, au labda nilionekana kuwa mtu wa kujali shughuli zilizokuwepo tu?

Haya maswali si mabaya kutumia tukijihoji kwa sababu sisi sote tuna madhaifu yanayoweza kugusa watu wengine.  Ndiyo maana tunahitaji kuungwa mkono na kuwa na chanzo cha uwezo wa kutubadilisha, tuwe mtu aliye tofauti machoni mwa watu wengine wakati tunakutana, bila hata kufikiria.  Kwa hiyo …

Warumi 15:13  Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.

Ukweli usiopingika:  Tumaini lake Mungu, furaha ya Mungu, amani ya Mungu, hayo yote yanaonekana ndani yetu moja kwa moja wakati tunamwamini.  Si hisia zinazopendeza kwa ndani tu, hata kama zinafurahisha, hapana.  Bali, Utapata kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu. 

Na hii itakubadilisha kabisa.  Pia, itabadilisha watu ambao unaenda kukutana nao.  Italeta mtikiso tofauti kwa maisha yao.  Hayo yote yatatokea wakati tunamwamini yeye. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy