... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Muongo Wewe!

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Yohana 2:3-6 Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, iikwa tunashika amri zake. Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake. Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.

Listen to the radio broadcast of

Muongo Wewe!


Download audio file

Wengi wetu tunatamani kuwa na maisha yaliyobadilika.  Kwa nini?  Ni kwa sababu hakuna aliyekamilika.Tunafahamu kwamba tunayo mapungufu na madhaifu.  Tungependa kuyashinda, ndiyo maana tunataka kuwa na maisha yaliyobadilika.

Mtu hawezi kuishi maisha bora kama bado ana uchungu moyoni kutokana na tukio lililotokea zamani; au kama anamwonea mwingine wivu; au kama hajasamehe mtu kutoka moyoni … au lo lote lile lingine, ni mengi.

Tunafahamu hayo lakini bado tunajikuta tumekwamia pale pale – tukishindwa kuachana nayo.  Sijui kama umeshaona hayo?

Mungu anatupenda sana, kama vile mzazi mwema apendavyo mwanae. hekima yake anayoitumia kwa kutusaidia kushinda mapungufu yetu ni sahihi kabisa, lakini watu wa tabaka zote bado wanalaumu dhana ya kumtii Mungu.

1 Yohana 2:3-6  Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake.  Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake.  Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli.  Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake.  Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.

Wakati ninafundisha habari ya kutii, watu wanasema mimi ni mtu wa sheria, Mfarisayo na kadhalika.  Sawa, haina shida, ukinishutumu ujue kwamba mimi ni mwenye kupeleka ujumbe tu.

Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake.  Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli.    

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy