... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Muujiza Mkubwa Kuliko Yote

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Petro 1:15,16 Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.

Listen to the radio broadcast of

Muujiza Mkubwa Kuliko Yote


Download audio file

Ebu fikiria kwamba umeona kikombe cha dhahabu kwenye takataka.  Unakichukua – halafu ni kichafu sana, hakipendezi. hatimaye unaanzia kukisafisha hadi kinaang’aa na kuwa dhahabu safi kabisa. Yaani, kinapendeza!  Lakini sasa, utakitumiaje?

Nijibu sasa, Kikombe kile utakitumiaje?, utakiweka ndani ya kabati ya maonyesho ili kiendelee kuwa kisafi na kubaki katika hali ya usalama?. Lakini Mungu yeye atakitumiaje?  Tayari tumeshajua jibu la swali letu, kwasababu tunafahamu yale aliyoyatufanyia wewe na mimi, baada ya kutuona kwenye jalala na kutusafisha. Anatutupa pale pale alipotuona mwanzoni.  Hii ni kweli? 

Mwinjilisti wa karne ya ishirini aitwaye Leonard Ravenhill, akiwa mwandishi alisema hivi:  Muujiza mkubwa kuliko yote ambayo Mungu angefanya leo ni kumchukua mtu asiye mtakatifu na kumfanya kuwa mtakatifu, halafu baadae amrudishe tena pale pale kwenye ulimwengu mchafu na kumlinda ili asichafuke. 

Yaani, mpango wa Mungu daima ulikuwa ni kukuokoa, kubadilisha maisha yako, kukutakasa uwe safi, halafu akurudisha pale pale katika machafuko ya dunia hii hii ili akutumie, uweze kumtoa mwingine atoke kwenye uchafu wake. 

Lakini kuna hatari, Wakati unarudishwa pale ni rahisi kupoteza mng’ao wako licha ya kuwa mtakatifu kwa ndani, na hatimaye utarudi kufanana nao kwa nje.  Kwa hiyo leo nakupa neno la tahadhari: 

1 Petro 1:15,16  Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. 

Usikubali dhambi ya ulimwengu huu ukuchafue tena.  Ubaki kuwa mtakatifu kwa maana Bwana Mungu wako ni mtakatifu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy