... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Muumba Aliyekataliwa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 1:10,11 Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua. Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.

Listen to the radio broadcast of

Muumba Aliyekataliwa


Download audio file

Krismasi imekaribia sana, na kwa watu wengi, swala la Yesu linapuuzwa tu – hawamjali.  Ni kuendelea tu na mambo ya sherehe kama vile mapambo ya mti wa Krismasi, vyakula vitamu na kadhalika … hatimaye itapita, basi.

Nilikutana na mtu aitwaye Anderea.  Aliniuliza kazi yangu.  Kwa hiyo nilimwambia, “Mimi ni mtumishi wa Mungu”.  Mara moja alikunja uso wake na kunijibu, “Aha, mimi siwezi kuamini ile takataka.  Ni hadithi tu, si kweli.”

Badala ya kukwazika, nilimwonea huruma kabisa.  Kwa sababu ndivyo mimi nilivyofikiri miaka mingi iliyopita.  Na ndivyo ulimwengu umemwitikia Yesu miaka yote elfu mbili iliyopita.  Mtume Yohana aliandika hivi …

Yohana 1:10,11  Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua.  Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.

Labda wewe unafanana na huyo Anderea. Ukiwa kama yeye, jua ya kwamba ninakuombea kama vile ninamwombea Anderea.  Kwa sababu Yesu yupo kweli kweli.  Anakupenda.  Alikuja ili akuokoe.  Dua langu ni kwamba ungemjua kama Mwokozi na Bwana wa maisha yako.  Hatima yako ya milele inategemea ujuzi huo!

Au pengine, tayari umeshamjua Yesu lakini unafahamiana na mtu aliye kama Anderea.  Tafadhali umwombee mtu yule kila siku na Bwana akikupa nafasi, mshirikishe yale ambayo Yesu amekutendea katika maisha yako.  Hatima yake ya milele inategemea ujuzi huo.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy