Nadharia Yahusuyo Mkokoteni
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wakolosai 3:22 Ninyi watumwa, watiini hao ambao kwa mwili ni bwana zenu, katika mambo yote, si kwa utumwa wa macho, kama wajipendekezao kwa wanadamu, bali kwa unyofu wa moyo, mkimcha Bwana.
Labda utafikiri kwamba nimechanganyikiwa lakini mimi naona kama swala la kurudhisha mkokoteni mdogo ni mtihani unaompima mtu kuona kama anaweza kufanya yaliyo haki. Kwasababu kama sisi si walemavu, zoezi la kurudisha mkokoteni sehemu yake ni kazi ndogo tena rahisi, tendo ambalo sote tunajua kwamba ni sahihi.
Hata kama si kosa la jinai kuuacha popote pale kwenye maegesho ya magari kitu ambacho hakuna atakayekuadhibu wala kukupiga faini,
Sasa ule muda wa kufanya maamuzi huku ukijiuliza je, nikirudishe au nikiache tu popote pale? – kumbe kila kikapu cha kuwekea vitu kinatufundisha mengi kuhusu tabia yetu. Je! Nitafanya yaliyo sahihi bila kushurutishwa? Je! Nitarahisisha wafanyakazi mahali pale na hata wateja wanaoendelea kufika mahali pale kwa unyofu wa moyo wangu … au la?
Labda utafikiri, haina shida. Hakuna atakayeniona.
Wakolosai 3:22 Ninyi watumwa, watiini hao ambao kwa mwili ni bwana zenu, katika mambo yote, si kwa utumwa wa macho, kama wajipendekezao kwa wanadamu, bali kwa unyofu wa moyo, mkimcha Bwana.
Kila siku, tuna fursa wewe na mimi ya kufanya yaliyo mema, yaliyo sahihi kwa njia nyingi ndogo ndogo ambazo wengine hawataona. Swali lililopo ni hili … Je! Tutachukua fursa hizo?
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.