Nafasi ya Kujirekebisha
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
2 Petro 1:3,4 Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.
Siku hizi hapa kwetu, mtu akinunua fanicha mpya, inakuja ndani ya box bapa na inatakiwa mnunuzi akusanye vipande vilivyomo na kuvifungia pamoja na bolt yeye mwenyewe. Lakini kama wewe si fundi kama mimi nilivyo, jamani, ile box inatisha sana!
Sasa, meza yangu ya kujisomea, ilikuja hivi ndani ya ma-box . Pia iliambatana na kabati ya ukutani na droo kadhaa na vyote vilitakiwa viunganishwe pamoja na kufungwa vizuri ukutani visiniangukie na kuniumiza.
Kwa bahati ninafahamiana na fundi aitwaye Harry. Bila yeye, nadhani vipande vile vyote vingekuwa bado chini ndani ya zile box tatu.
Lakini hapo hapo kuna habari njema.
2 Petro 1:3,4 Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.
Sio lazima wewe mwenyewe ujaribu kuunganisha maisha haya mapya kwa nguvu zako mwenyeewe. Sio lazima. Kwa sababu Yesu ndiye anayotumia uweza wa Mungu na kwa kutukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.