... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Nakupenda Sana

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 18:1,2 Wewe, BWANA, nguvu zangu, nakupenda sana; BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia.

Listen to the radio broadcast of

Nakupenda Sana


Download audio file

Nadhani hakuna kitu kinachotisha kabisa kama tetemeko la ardhi.  Yaani ardhi chini ya miguu yako inayumba-yumba, wewe ukingoja jengo likuangukie pande zote na kukuseta chini ya mabomoko.

Taarifa ya sayansi kwenye mtandao inaeleza kwamba tetemeko la ardhi kubwa iliyowahi kupimwa dunani ilitokea May 22, 1960 kwenye mji wa Valdivia, nchini Chile.  Ilipimwa nguvu ya 9.5 kwenye Kipimo cha Richter.  Watu takriban 1,655 walikufa, maelfu wengine waliumia vibaya na watu ma-miliyoni walibaki bila makazi. 

Tunatazamia ardhi kuwa imara sana chini ya miguu yetu.  Na tunashukuru kwamba kawaida iko hivyo.  Ni bahati kwamba matukio ya majanga ya kutetemeshwa kwa ardhi hua yanatokea mara chache.  Ila matukio mengine yanayotutikisa vibaya maishani, yenyewe si mara haba.

Kinachohitajika kipindi kama hicho, wakati misingi wa maisha yetu inatikiswa chini ya miguu yetu, wakati yote tuliyoshughulikia na kujenga yakibomoka na kuhatarisha hata uhai wetu … kinachohitajika zaidi ni kuwa na msingi imara chini ya miguu yetu.

Zaburi 18:1,2  Wewe, BWANA, nguvu zangu, nakupenda sana; BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia.

Na wewe pia umruhusu Mungu awe Mwamba wako.

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy