... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Namna ya Kuutambua Uongo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 8:31,44 Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli ... Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.

Listen to the radio broadcast of

Namna ya Kuutambua Uongo


Download audio file

Siku hizi tumezungukwa na udanganyifu kila mahali, ni kweli, tangu miaka zamani watangazaji pamoja na wahariri wa vyombo vya habari wameegamia upande ule wanaopenda, lakini siku hizi sasa, habari za uongo zimeenea kupita kiasi, inazidi kuwa vigumu kupambanua na kujua kweli uko wapi ndani ya wingi wa uongo unaotangazwa.

Hatari hii si kwenye vyombo vya habari tu, Huwa inatokea hata katika maisha yetu sisi wenyewe.  Kwani, ni mara ngapi umebembelezwa na mtu anayejifanya kuwa rafiki yako lakini lengo lake ni kujinufaisha kupitia wewe?

Sasa mtu atawezaje kuugundua uongo ukimjia?

Yohana 8:31,44  Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli … Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda.  Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake.  Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.

Kama tumemsikia Yesu vizuri, njia ya kutambua uongo ni kwa kuijua kweli.  Njia ya kugundua uongo ni kumsikiliza yeye, kupokea mafundisho yake na kuyatii.  Kwa sababu Ibilisi anahakikisha kwamba ulimwengu umejaa uongo tu.  Lakini uongo unazidi kudhihirika na kuwa rahisi kuupambanua pale ukweli wa mafundisho ya Yesu unapojaa moyo wako.

Mfuate Yesu.  Yakubali na kutii mafundisho yake.  Ndipo utajua kweli; na kweli hiyo itakuweka huru.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy