Ndani ya Kitovu cha Dhoruba
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 46:1-3,10 Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, ijapopepesuka milima kwa kiburi chake ... Acheni, mjue ya kuwa mimi ni Mungu, nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi,
Kuna mambo huwa yanatokea maishani ambayo yanatisha kweli. Wakati mwingine, maisha yanatushurutisha kufanya kazi hadi mtu anachoka kabisa. Hata iweje, kinachohitajika ni kupata amani. Sasa, niambie, amani hiyo itatoka wapi?
Wakati matukio ya maisha yanakutikisa vibaya, ni vigumu mno kushikilia amani. Mtu atawezaje kuwa na amani moyoni wakati uchumi unaporomoka, ndoa inaharibika, mtoto anakuwa mkaidi, mtu unatoka kupima hospitali halafu unaambiwa una ugonjwa usiotibika?
Mara nyingi, tunajaribu kutumia akili zetu na kurudia mawazo ya kutatua tatizo, hata usiku tunapojigeuza kitandani huwa tunakosa kabisa kuwa na amani. Je! Kufanya hivyo imewahi kukusaidia.
Sikiliza maono ya Mungu kuhusu swala hilo, kuhusu kweli na amani yake.
Zaburi 46:1-3,10 Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, ijapopepesuka milima kwa kiburi chake … Acheni, mjue ya kuwa mimi ni Mungu, nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.
Nchi inabadilika, milima inatetemka baharini, bahari nayo inavuma, ardhi inatetemeka chini ya miguu yako. Huwezi kupata jibu kwenye mtandao, hapana! Mahali panapotupasa mimi na wewe kuwepo ni mahali pa usalama; si kutoka kwenye misukosuko hiyo tu!, bali ni kubaki ndani ya kitovu cha dhoruba kwa sababu ndipo alipo Mungu.
Acheni, mjue ya kuwa mimi ni Mungu, nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.