Ndivyo Mabadiliko Yanavyokuja
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Isaya 55:8-11 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.
Kadiri matukio yanavyotokea duniani – kama ni vita au kama ni watu mashuhuri wakijionyesha kwenye tamasha – wakati sisi watu wa kawaida tunazidi kupambana na changamoto za maisha, ni vigumu kuwa na uhakika kwamba kuna Mungu wa upendo ambaye anaongoza vyote vinavyoendelea ulimwenguni. Baadhi ya watu wanaona kwamba hakuna Mungu aongozaye.
Kwa kweli kwangu mimi, kwa miaka mingi sikuweza kukubali kama kuna Mungu atawalaye. Yaani dhana hizi mbili – kuzingatia vurugu za dunia hii na kwa upande mwingine kutafakari habari ya Mungu mwenye upendo wote ambaye ana uwezo wote – haziendani hata kidogo hadi kuonekana kuwa kichekesho.
Kwa nini tusimpe Mungu nafasi kujieleza katika kipindi chetu hiki kwa siku ya leo?
Isaya 55:8-11 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.
Hatupendi dhoruba lakini bila dhoruba ziletazo mvua, hatutapata chakula. Na hata kama njia zake Mungu hazichunguziki, akitamka neno, mambo yanaanza kutokea. Wakati Mungu anaongea na nafsi zetu, jamani, jua kwamba mabadiliko yanakuja!
Kwa hiyo, jihurumie tafadhali. Mruhusu Mungu aongee nawe akuletee pendo lake na uwezo wake maishani mwako, hata siku zile ambazo unajikuta umechanganikiwa.
Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.