Neema na Amani
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Wakorintho 1:3 Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.
Ukikutana na mtu ambaye ni siku nyingi hamuonani, je! Unamsalimiaje? Au wakati unamwandikia barua (labda siku hizi, barua pepe), unaanzaje?
Agano Jipya kwa sehemu, ni mkusanyo wa nyaraka zilizoandikwa na watu kama Paulo na Petro, wakiwaandikia Wakristo, baadhi yao wakiwa wanateswa, wengine wakipotoshwa, wote wakikumbana na changamoto mbali mbali na mazingira tofauti tofauti.
Ila walikuwa wote na changamoto kubwa moja – dunia ya kale ilikuwa sehemu iliyotawaliwa na ukatili, ukizingatia kwamba Warumi walikuwa wameeneza ukoloni wao kote kote, wafalme wao madikteta walioitwa Kaisari, wakitawala kimabavu na kwa dalili ya wazimu wakijiita kuwa mungu.
Kwa kweli ilikuwa kipindi kibaya cha kinyama. Sasa katika mazingira kama haya, tunashangaa kuona ndani ya nyaraka zile za Agano Jipya, jinsi walikuwa wamezoea kusalimiana, kama vile Mtume Paulo aliyotumia katika mstari ufuatao:
1 Wakorintho 1:3 Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.
Mtu akizingatia mazingira yale walimoishi, atajua kwamba si maneno ya mazoea tu. Walikuwa wanamaanisha kweli kweli maneno yaliyofaa kwa wakati ule. Sasa tuulize, Je! Neema ile na amani ile ziliwafikia kutoka wapi? Kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo. Na hata kwa sisi ni vivyo hivyo.
Hii ndiyo baraka Mungu ameandaa kwa ajili yako. Ndiyo aliyokusudia upite katikati ya mazingira yako magumu, majaribu unayoyapata.
Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.