Neno la Kutafakari
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Warumi 5:6-8 Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema. Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.
Tukielekeza mawazo yetu kwenye Krismasi, tunakuta kuna jambo ambalo, kwa watu wengi, linakuwa kizuizi wasiweze kufurahia sherehe hii ya Krismasi kama ipasavyo.
Kwa miaka mingi, nilihofia sana Krismasi, nadhani ni kwa sababu siku ile ilikuwa inamulika mwenendo wangu kama ulivyokuwa – ila wakati ule nisingeweza kueleza hivyo. Kwa kuwa nilihisi kwamba sikustahili.
Moyoni, nilihisi kwamba habari hii yote ni ya kweli – kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, aliyezaliwa kwa umbo la kibinadamu na hatimaye kugongomewa msalabani kulipa deni la dhambi zangu zote ili Mungu aweze kunisamehe.
Lakini kwa kuwa mwenendo wangu haukuwa mzuri, sikupenda kumulikwa na ukweli huo. Kwa hiyo mwitikio wangu dhidi ya Krismas ulikuwa wa aibu na kuona kwamba sifai kabisa. Ninajiuliza,! Wewe unajionaje ukitafakari maana ya Krismas?
Warumi 5:6-8 Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema. Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.
Kwa kweli ni neno la kutafakari sana kwa sababu …
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.