Nguvu ya Moyo Wako
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 73:25,26 Ni nani niliye naye mbinguni, wala duniani sina cha kupendeza ila Wewe. Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu na sehemu yangu milele.
Dalili ya mtu aliyekomaa ni wakati anajifunza kutokujitegemea. Sisemi awe na mtazamo hasi, hapana, bali akubaliane na madhaifu na mapungufu yake. Hii ni busara ya mtu aliyekomaa.
Sijui wewe ulikuaje, lakini wakati mimi nilikuwa kijana, niliamini kwamba hata risasi haiwezi kuniua. Niliendesha gari langu kasi kabisa kwenye barabara zilizokuwa nje ya mji, na kama nilifaulu kuirusha juu nikipitia tuta, kwa kweli nilifurahi. Naamini kwamba hukupumbazika hivi kama mimi. Nikiangalia nyuma, ninashangaa kuona kwamba bado mimi niko hai leo.
Tukiwa vijana, tunajitegemea sana. Tunajiamini kupita kiasi. Lakini kadiri mtu anakua, kupitia changamoto za maisha, anafundishwa hekima ya kuelewa kwamba anaweza kuuawa na risasi; kwamba watu wote wana madhaifu na mapungufu ya asili.
Busara hii aliipata mtunga zaburi huyu aliyeandika mistari inayofuata kwa kupitia matukio ya maisha yake:
Zaburi 73:25,26 Ni nani niliye naye mbinguni, wala duniani sina cha kupendeza ila Wewe. Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu na sehemu yangu milele.
Ni kweli, mwili na moyo hua inapunguka lakini bado tunaweza kuendelea kujifunza kwamba utukufu wake Mungu, kwa kupitia neema yake na pendo lake kubwa kwetu sisi, anaweza kuwa mwamba wa mioyo yetu na sehemu yetu … milele. Usijaribu kupambana peke yako.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.