Nguvu Zinatoka kwa Mungu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 62:10,11 Msiitumainie dhuluma, wala msijivune kwa unyang’anyi; mali izidipo msiiangalie sana moyoni. Mara moja amenena Mungu; mara mbili nimeyasikia haya, ya kuwa nguvu zina Mungu.
Kuna kipindi maishani hata tukijitahidi, hata tukajitolea kwa nguvu gani mambo hayaendi kabisa. Yaani hatuoni pa kupitia na kusongambele. … ndipo tunaweza kupumbazika na kufanya mambo ya ajabu ajabu.
Labda umejisikia kwamba unagonga kichwa ukutani tu, ukishindwa kupiga hatua yo yote, ukijitahidi kukamilisha mambo yako lakini wapi, hamna kitu. Sasa, mtu atafanyaje?
Wengine wanaendelea kugonga kichwa ukutani pale pale kana kwamba kutatokea mabadiliko. Haieleweki, wala siyo busara, lakini sote nadhani tumekaidi hivyo, si kweli?
Pia, kuna wakati tunajichukulia maamuzi bila kujali watu wengine hata kama tunaanza kuwakamdamiza na kuvunja mahusiano tukisema – Acha, uhusiano ule utanisaidia nini! Kwa kweli, inatisha kukiri kwamba tunaweza kufiri hivyo … lakini hua inatokea. Au labda tunaweza kutumia uongo kidogo hapa na pale na kupinda kweli.
Wengine wanao uwezo wa kutapanya pesa kwa kutatua tatizo, kwa hiyo wanafanya hivyo. Yaani kuna mbinu nyingi za kujaribu kupenya na kufika upande wa pili! Tunataka yale tunayoyataka, basi! Na kama nilishasema, tunaweza kufanya mambo ya upumbavu kweli.
Lakini ingekuaje kama kuna njia badala? Kubali, usikubali, ipo kabisa … tena ni bora kuliko tulivyofikiria:
Zaburi 62:10,11 Msiitumainie dhuluma, wala msijivune kwa unyang’anyi; mali izidipo msiiangalie sana moyoni. Mara moja amenena Mungu; mara mbili nimeyasikia haya, ya kuwa nguvu zina Mungu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.