... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ni Jambo la Kufedhehesha Kweli

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 7:12 Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.

Listen to the radio broadcast of

Ni Jambo la Kufedhehesha Kweli


Download audio file

 Kwa miaka mingi sasa, nimekutana na watu wengi wanaoishi kwenye nchi ambazo mtu hana uhuru wa kutoa mawazo yake.  Huwa ninawasikitikia sana  namna wanavyoonewa.

Uhuru wa kutamka wazi ni jambo ambalo wengi wetu tunaona kuwa ni haki ya kimsingi ya kibinadamu. Lakini leo kwenye jamii ambazo wanapojidai kuwa wenye mawazo huru, uhuru huo unaanza kumomonyoka haraka asana kuliko tulivyofikiria,  Zamani, mheshimiwa Winston Churchill alitaabiri hivi: 

“Dhana ya watu baadhi kuhusu uhuru wa kusema ni kwamba, wao wako huru kuongea kama wanavyotaka, lakini mtu mwingine akiwahoji, wanasema kwamba anataka kuwafedhehesha.” 

Na ndivyo imekuwa siku hizi katika majadiliano ya jamii.  Hakuna tena adabu, kuheshimiana, wala upendo.  Imebaki tu mabishano ya watu wenye misimamo inayopingana, kila upande ukijaribu kutafuta ushindi.

Mapambano hayo mara nyingi yanalenga Ukristo na imani zetu wewe na mimi, ndani ya Yesu, wakipinga msimamo wetu wa kutenganisha yale ambayo Mungu anasema ni mema au mabaya.  Wapinzani wetu wanajaribu kutunyamazisha tusitamke ukweli.  Sasa, mwitikio wetu uweje?  Je!  Tuwapigie kelele na sisi kwa upande wetu? 

Sidhani.  Yesu alisema hivi: 

Mathayo 7:12  Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii. 

Kwahiyo, ungependa iweje?  Ungependa wapinzani wako, wale walio kinyume chako kabisa, wanaokukosoa na kukudhalilisha … Je!  Ungetaka wakutendeeje? 

Basi, ndivyo Yesu anataka uwatendee wapinzani wako na watu walio kinyume chako. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo. 


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy