Ni Kiumbe Hai
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 24:11,12 Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe; nao walio tayari kuchinjwa uwaopoe. Ukisema, Sisi hatukujua hayo; Je! Yeye apimaye mioyo siye afahamuye? Naye alilindaye nafsi yako siye ajuaye? Je! Hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake?
Tukitumia mfano wa vita, eneo la mapambano makali; kati ya watu wa ulimwengu na wa Yesu kuhusu swala ya kutoa mimba. Waulimwengu wanauliza, Kwanini Wakristo wanaonekana wamepitwa na wakati kuhusu ishu hiyo?
Kusema ukweli; kabla sijabadilika kuwa Mkristo nikiwa na umri wa miaka 36, sikuona ubaya wowote kwenye swala la kutoa mimba. Shida iko wapi? Ni wazi kwamba, watu wanaotoa mimba wao wanaona ni bora kutoa mimba kuliko kumleta mtoto ambaye hawakumtaka kwa wakati huo. Kwa nini Wakristo wamekwamia sana kwa ishu hiyo?
Lakini dakika ile nilipokabidhi maisha yangu kwa Kristo, bila hata kufikiria, mtazamo wangu ulibadilishwa. Niliweza kuchunguza swala hilo na kuona ukweli uko wapi. Kama vile Kevin Sorbo wa shirikia la Vitae Foundation alivyosema, “Kwa siku ya 22 baada ya mimba kuchukuliwa, tayari kuna mpigo wa moyo. Sasa kama si dalili ya uhai, basi niambie ni kitu gani?” Amesema kweli kabisa!
Kwahiyo, baada ya kusimamia pande zote mbili kwa vipindi tofauti katika maisha yangu, ninaweza kuwaelewa wote, wanaotetea uamuzi wa kutoa mimba na wanaotetea uhai. Ninawaelewa. Lakini kwanini Wakristo wasiridhike kubaki na maoni yao bila kupaza sauti kwa kuyatetea?
Mithali 24:11,12 Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe; nao walio tayari kuchinjwa uwaopoe. Ukisema, Sisi hatukujua hayo; Je! Yeye apimaye mioyo siye afahamuye? Naye alilindaye nafsi yako siye ajuaye? Je! Hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake?
Ni kwa sababu kutoa mimba ni kuua. Halafu sisi tunaomwamini Yesu, hatuwezi kutulia na kunyamanza tu. Mimba ile … ni uhai. Na tukipata nafasi, lazima tufanye yale tuwezayo kuuokoa.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.