Nifuate
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mariko 2:13,14 Akatoka tena, akaenda kando ya bahari, mkutano wote ukamwendea, akawafundisha. Hata alipokuwa akipita, akamwona Lawi wa Alfayo, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate. Akaondoka akamfuata.
Nadhani sio mimi peke yangu ambaye angekiri kwamba kuna wakati nimejiona kuwa sifai kabisa, kiasi cha kutatishwa tamaa na kuacha kufuata ndoto nilizokuwa nazo. Sijui wewe?
Changamoto zinaonekana kuwa kubwa mno wakati sisi wenyewe tunajiona kuwa wadogo sana. Isitoshe, tunafahama vizuri kwamba tumewahi kukosea mara nyingi, kwa hiyo mtazamo wetu hasi unasabisha tulemazwe tusiendelee mbele.
Sasa fikiria ingekuwaje, pamoja na mtazamo kama huo, ikiwa unajua kwamba wanaokuzunguka wanakuchukia sana! Ilikuwa hivi kwa mtoza ushuru Myahudi, Lawi, zamani kwenye karne ya kwanza. Wayahudi walichukia sana watoza ushuru kwa sababu walishirikiana na ukoloni wa Warumi kusumbua wananchi wenzao, wakizidisha kodi kwa kujinufaisha pia.
Halafu Yesu alikuja, ambaye tukisema kweli, alikuwa maarufu sana, akafika mahali pale.
Mariko 2:13,14 Akatoka tena, akaenda kando ya bahari, mkutano wote ukamwendea, akawafundisha. Hata alipokuwa akipita, akamwona Lawi wa Alfayo, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate. Akaondoka akamfuata.
Zamani, wakati ule, kama mtu alitaka kufuata rabbi, yaani mwalimu, ilibidi apeleke kwanza ombi; halafu aonyeshe kwamba ana sifa za kuwa mmoja wa wanafunzi wake. Ilibidi pia awe ametoka kwenye ukoo wenye sifa njema. Lakini hapa tunaona huyu Yesu aliyefuatwa na umati mkubwa wa watu, akipindua mambo na utamaduni, akamwambia Lawi – “Nifuate.”
Sasa wewe, katika mtazamo wako hasi, kama umesita kumfuata Yesu kwa kuona kwamba hufai, jua hili: Alikuja kwa ajili ya watu kama wewe.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.