Nikitafakari
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 119:59,60 Nalizitafakari njia zangu, na miguu yangu nalizielekezea shuhuda zako. Nalifanya haraka wala sikukawia, kuyatii maagizo yako.
Nina swali kwako leo: Je! Ni mara ngapi unatafakari namna unavyoishi? Ni mara ngapi unatafakari muitikio wako dhidi ya mazingira mbalimbali, na vichangamsho, vikiwa vizuri au vibaya ambavyo unakutana navyo maishani?
Ni maswali muhimu sana, kwa sababu ukiamka kila siku ukiwa na mwitikio ule ule dhidi ya matukio – aidha yawe mema au mabaya – basi, hakuna yatakayobadilika.
Kama tunafikiri kwamba mambo hayawezi kuboreka watu wengine wasipobadilika, au mazingira yabadilike kwanza – ni kwamba tutasubiri weeeh kwasababu inawezekana hakuna kitakachobadilika. Sasa jibu litatoka wapi?
Zaburi 119:59,60 Nalizitafakari njia zangu, na miguu yangu nalizielekezea shuhuda zako. Nalifanya haraka wala sikukawia, kuyatii maagizo yako.
Acha nirudie swali langu la awali. Je! Ni mara ngapi unatafakari njia zako? Kwasababu, kila ninapofungua Kitabu Kizuri, yaani Biblia, na kusoma ndani ya Neno la Mungu, yeye anasababisha nitafakari njia zangu. Anamurika nuru yake, utukufu wake, uweza wake, upendo wake, furaha yake na amani yake ndani ya kila kona ya moyo wangu.
Nikitikiswa hivyo, ninapata shauku kubwa moyoni mwangu ya kumheshimu, kumtii na kuelekeza miguu yangu kwenye shuhuda zake.
Yaani, tendo la kusoma Biblia kila siku na kumsikiliza Mungu na kutafakari njia zangu kwenye nuru ya Neno lake, yananiwahisha kutii maagizo yake.
Ndivyo inavyotakiwa. Ndio njia ambayo Mungu anaitumia kwa kutubadilisha. Ndivyo anavyobadilisha maisha yetu. Ndiyo mambo yanavyoweza kuwa bora hata kama watu wengine hawabadiliki, wala mazingira yetu hayabadiliki.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.