... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Nina Wewe Tu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 73:25,26 Ni nani niliye naye mbinguni, wala duniani sina cha kupendeza ila Wewe. Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu na sehemu yangu milele.

Listen to the radio broadcast of

Nina Wewe Tu


Download audio file

Acha nikuulize, ni mambo gani matatu makubwa ambayo huwa unayaombea sana?  Yawezekana ni afya njema, kufanikiwa kiuchumi, au ndoa yako iboreke.  Taja vipaumbele vyako.

Hapa kwenye huduma yetu ya Christianityworks yaani Ukristo Unatenda Kazi Kweli, tuna tovuti iitwayo PowerfufPrayer.org yaani Maombi yenye Nguvu.  Kwa nini tunasema “maombi yenye nguvu”?  Ni kwa sababu Biblia haionyeshi aina nyingine ya maombi isipokuwa maombi yaletayo mabadiliko yenye nguvu.  Ni kweli kabisa!  na watu wengi wanaleta mahitaji yao kwenye tovuti yetu na wengine wanapokea kila wiki, barua pepe ya kuombea watu kadhaa kwa idadi waliojichagua wenyewe.  Unaweza kuangalia mwenyewe kwenye tovuti yetu ya PowerfulPrayer.org. 

Ni wazi kwamba huwa tunapokea aina nyingi sana za mahitaji ya kuombea.  Na kweli, watu wengi wana matatizo makubwa – ndoa zinavunjika kwasababu ya uasherati, familia zinasambaratika wakikimbia vita. Tunawaombea watu wengine na kujaribu kuwatia moyo.  Hii ni sahihi na tunapaswa kuendelea kuombea mahitaji hayo. 

Lakini kuna hitaji moja ambalo huwa tunaliombea mara chache sana. Nalo ni hili Nataka nimsogelee zaidi Yesu.  Kwa nini ombi hilo linaonekana kwa nadra sana?  Sikia alivyoandika mtunga Zaburi: 

Zaburi 73:25,26  Ni nani niliye naye mbinguni, wala duniani sina cha kupendeza ila Wewe.  Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu na sehemu yangu milele. 

Ndio, endelea kuombea mahitaji yako ya hapa duniani. Lakini kila kitu kwenye maisha yetu ya hapa chini kinamwisho, ipo siku kitatoweka. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy