... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Pale Shida Zinapobadilika na Kuwa Miujiza

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 2:1-3 Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo. Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake. Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai.

Listen to the radio broadcast of

Pale Shida Zinapobadilika na Kuwa Miujiza


Download audio file

Kawaida maisha huwa yanaendelea tu, mtu akifanya kazi ile ile siku baada ya siku.  Kama vile mshauri wangu mmoja mwenye busara anavyopenda kusema, Kuna siku zingine inabidi uendelee kujikokota kwa ajili ya Mungu.  Lakini kuna wakati utajikuta unasimama mbele ya ukuta mrefu.

Sasa, inapotokea hivyo mtu afanye nini?,  Hii ilitokea zamani wakati Yesu alipokuwa hapa duniani.

Yohana 2:1-3  Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo.  Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.  Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai.

Yaani ilikuwa aibu!  Ebu fikiria kutindikiwa vinwaji siku ya arusi!  Na kama ulishasoma habari hiyo, ni kama Yesu hakujali saana.  Halafu kama mwana mwema, alifanya kama mama yake mzazi alivyoomba.  Cha ajabu sasa!  Alibadilisha maji kuwa divai, tena si machache, lakini karibia galoni 150 ya divai!

Tunajifunza nini hapo?  Tunataka kuelewa nini kutokana na muujiza huu wenye uwezo wa kutusaidia katika maisha ya kila siku?  Mimi ninaona hivi:  Kila muujiza ndani ya Biblia ulianzia kwenye tatizo fulani.  Baadaye, Mungu anaingilia kati na uwezo wake wa ki-Mungu na kubadilisha mfumo wa kawaida ili aonyeshe uwezo na utukufu wake.

Kwa vyovyote, endelea kujikokota mbeleni taratibu taratibu kwa ajili ya Mungu. Lakini utakapokumbana na ukuta ule mkubwa, yaani tatizo lisilotatuliwa, basi mwambie Yesu kwamba umetindikiwa divai … halafu wewe subiri matokeo! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.