Pendo Halipotei Bure
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mathayo 27:27-31 Ndipo askari wa liwali wakamchukua Yesu ndani ya Praitorio, wakamkusanyikia kikosi kizima. Wakamvua nguo, wakamvika vazi jekundu. Wakasokota taji ya miiba, wakaiweka juu ya kichwa chake, na mwanzi katika mkono wake wa kuume; wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki, wakisema, Salamu, Mfalme wa Wayahudi! Kisha wakamtemea mate, wakautwaa ule mwanzi, wakampiga-piga kichwani. Walipokwisha kumdhihaki, wakalivua lile vazi, wakamvika mavazi yake, wakamchukua kumsulibisha.
Je! Umewahi kumtendea mema mtu fulani halafu ulichukia wakati hakukutambua wala kukushukuru? Ikitokea, kwa kweli mtu anabaki kwa kujiuliza, Faida gani nimepata kumsaidia Huyu?
Watu kukosa shukrani na mwitikio wetu hua inadhihirisha kilichomo moyoni mwetu. Si inaonyesha kiburi chetu wakati tunafikiri thamani la tendo letu jema linashuka hata kufutwa wakati mtu halitambui wala kulishukuru?
Dhana kwamba tendo jema lina thamani lenyewe licha ya mwitikio wa yule aliyetendewa imeenda wapi? Kwamba upendo ni rasilimali yenye thamani kuliko vyote, hata mlengwa hapokei upendo wetu, au hauelewi, au hauutambui?
Je! Leo hii, kuna mtu ye yote yule ambaye unayechoswa naye kwa sababu haelewi mema unayomtendea? Sikiliza mwitikio wa Yesu kwa wenye dhambi kama wewe na mimi, watu wazito wa kuelewa.
Mathayo 27:27-31 Ndipo askari wa liwali wakamchukua Yesu ndani ya Praitorio, wakamkusanyikia kikosi kizima. Wakamvua nguo, wakamvika vazi jekundu. Wakasokota taji ya miiba, wakaiweka juu ya kichwa chake, na mwanzi katika mkono wake wa kuume; wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki, wakisema, Salamu, Mfalme wa Wayahudi! Kisha wakamtemea mate, wakautwaa ule mwanzi, wakampiga-piga kichwani. Walipokwisha kumdhihaki, wakalivua lile vazi, wakamvika mavazi yake, wakamchukua kumsulibisha.
C.S. Lewis alieleza hivi: “Kamwe pendo halipotei bure, kwa sababu thamani yake haitokani na swala la kutendeana.” Tunapenda kwa sababu Mungu alitupenda kwanza.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.