... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Piga Mbio Katika Mashindano

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waebrania 12:1 Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu.

Listen to the radio broadcast of

Piga Mbio Katika Mashindano


Download audio file

Katika maisha haya, kuna wakati kila mmoja wetu anataka kuacha majukumu na kujiudhuru.  Inaweza kuwa katika ndoa yako, kazini ulipoajiriwa, hata safari yako ya imani.  Ujue kwamba si wewe tu.  Kuna nyakati nyingi sote tunataka kujiudhuru.

Niruhusu nikushuhudie kupitia kwangu kama mfano.  Miezi miwili na nusu iliyopita, nilifikia umri wa miaka 65 – umri ambao kwa kawaida watu wanastafu huku kwetu.  Halafu mara kwa mara, dhana ya “kustafu” inavuta mwili wangu.  Je!  Ni lazima niendelee kujitahidi hivi?  Kwa nini nisipumzike?

Lakini kila wakati, Mungu ananikumbusha  habari ya watu wasiohesabika, mamiliyoni kama wewe wanaohitaji kusikia habari za Yesu.  Wengi wao, wakipambana na mambo magumu.  Wengi wakivutwa na mfumo wa dunia hii.  Wengi ambao hawajapata fursa ya kusikia habari ya upendo wa Kristo uokoao.

Ni yapi Mungu ameweka mbele zako?  Ni mashindano gani unataka uyakimbie?  Halafu ni lini uliwahi kutaka kuacha yote na kujiudhuru?

Waebrania 12:1  Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu.

Angalia, mashindano ya kupiga mbio hayajaandaliwa kuwa rahisi au kwa ajili ya wao wanaopenda starehe.  Ugumu wake sio sababu ya kujiudhuru.  Angalia waliokutangulia, wanaokuzunguka, mashujaa wa imani unaowajua, ambao wanaendelea kupiga mbio licha ya lo lote lile.  Wakutie moyo kabisa uendelee na mashindano.

Halafu pia, ondoa katika maisha yako, cho chote kile kiwezacho kukukwamisha na dhambi ile inayokuangusha mara nyingi.  Piga mbio. Usiache.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.