Ratiba ya Mungu Haina Makosa
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Habakuki 2:3 Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.
Nikisema kweli, mara nyingi sikupendezwa na ratiba yake Mungu. Mara nyingi zaidi, mateso yaliendelea kupita kiasi. Halafu, mara nyingi sana amezuia baraka zake muda mrefu pia! Wewe unaonaje?
Nina rafiki kijana aliyeoa hivi karibuni na baada ya wao kufunga ndoa, mke wake alishikwa na ugonjwa wa kuishiwa nguvu daima. Kuugua ni kawaida lakini kwa nini Mungu anaruhusu hali hiyo iendelee tu?
Bila shaka wewe na mimi tungeweza kuorodhesha mifano mingi kama huo au mibaya zaidi, ambayo yanasababisha tumtilie Mungu mashaka. Kwa nini ratiba yake mara nyingi haieleweki kwetu?
Katika Agano la Kale, Nabii Habakuki naye pia alikuwa na malalamiko kama hayo.
Habakuki 1:2 Ee BWANA, nilie hata lini, wewe usitake kusikia? Nakulilia kwa sababu ya udhalimu, ila hutaki kuokoa.
Wakati ule mambo yaliwawia vigumu Waisraeli. Watu wa Babeli walikuwa wanaleta ghasia. Isingetushangaza kusikia Habakuki anavyomlilia Mungu. Jibu lake Mungu lilikuaje?
Habakuki 2:3 Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.
Ukizingatia mahali ulipo leo hii, sijui kama ni neno ambalo unalotaka kusikia. Inategemeana. Labda hutaki kuamini ahadi ile. Lakini subiri kwanza. Mungu anajua kabisa yale ambayo unayapitia. Na ni faraja kubwa kujua kwamba ratiba yake daima haina makosa.
Ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.
Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.