... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Saizi Moja Haiwezi Kuenea Watu Wote

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Warumi 12:4-6 Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa.

Listen to the radio broadcast of

Saizi Moja Haiwezi Kuenea Watu Wote


Download audio file

Nadhani sisi sote tumewahi kusumbuka sana wakati tunaongea na wakala au kupiga namba ya huduma kwa wateja – ikiwa benki, huduma ya umeme au maji, kampuni ya bima na kadhalika – wakati mwenye kuitika simu hawezi kutusaidia na kutatua tatizo tulilo nalo.  Yaani inaweza kutuchanganya mno, je, hii si kweli?

Mara nyingi haitakuwa kosa la mwenye kuitikia simu.  Yaani kampuni imemwekea mipaka ambayo inampasa kutumika ndani yake, pia mfumo wao wa komputa unawabana.  Ukitafakari kidogo, utaona kwamba shida ni makampuni yenyewe yanachukulia kana kwamba shida za wateja wote zinafanana tu, kwamba “saizi moja inawaenea wote” kama msemo ulivyo.

Lakini tukisema kweli, hata sisi ndivyo tunavyowachukulia watu wengine mara nyingi, kwa kuwalazimisha wacheze kufuatana na mpigo wetu wa ngoma na kuwawekea mipaka tuliyotengeneza sisi wenyewe kwa mtazamo wetu finyu, si kweli?

Ni mara ngapi ulitazamia mtu kuwa na mtazamo kama wa kwako na kuona kwamba amekuudhi wakati hakuwa nao au kwamba amekataa?  Ni wazi kwamba Mungu alituumba, kila mmoja wetu tofauti-tofauti, kwa hiyo lazima tuwe na mitazamo mbalimbali.  Inawezekana mtu kujua hayo, lakini bado inaweza kumchanganya.

Warumi 12:4-6  Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.  Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa.

Tafadhali, usiudhiwe na watu kwa sababu wako tofauti na wewe kwa kuwa ndivyo Mungu alikusudia na kila mmoja ni wa mwenzake.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.