... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Salama Zitokazo kwa Sosthene

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 1:1 Paulo, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu na Sosthene ndugu yetu.

Listen to the radio broadcast of

Salama Zitokazo kwa Sosthene


Download audio file

Tunaishi katika ulimwengu unaotukuza mashuhuri na mashujaa … warembo, matajiri, na mtu awaye wote aliyekusanya wafuasi wengi mwezi fulani kwenye mtandao … halafu sisi wengine tunabaki nyuma tu, hatujulikani.

Naamini kwamba sisi hatutafuti kutukuzwa  – kwa sababu ukiishi kwa kutafuta kujulikana, utajikuta unacheza kwa mpigo wa ngoma za watu wengine.  Lakini pia, haipendezi kupuuzwa.  Wengine wanaonekana sana lakini hakuna anayekuona wewe – hawaoni vipaji vyako, kujitolea kwako, mchango unaoweza kuleta.

Kuna jamaa moja katika Agano Jipya ambaye wengi wetu hatujawahi kusikika jina lake lakini bado anatajwa mle.

1 Wakorintho 1:1  Paulo, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu na Sosthene ndugu yetu.

Ni nani huyu Sosthene?  Ukisoma Matendo 18:17, utaona kwamba yeye alikuwa mkuu wa Sinagogi ya Wayahudi mjini Korintho, aliyepigwa sana mbele ya mkuu wa mkoa wakati kulitokea ghasia ya watu.  Hatujui zaidi lakini baada ya tukio lile la hatari, kumbe!  Tunamkuta njiani akisafiri na Mtume Paulo, mmoja wa mashuhuri katika Biblia.

Hata kama sisi hatujui mengi kuhusu Sosthene, wala hajulikani duniani, je!  Unadhani Mungu hakumjua?  Unafikiri Mungu hakuona alivyoteswa wala kuthamini mchango wake katika huduma?  Je!  Hujui kwamba sasa hivi yu mbele zake Bwana akipokea thawabu yake?

Ni kweli, hatuna mashuhuri wengi kati yetu machoni pa ulimwengu huu.  Hatukukusudiwa kujulikana sana.  Lakini hailishi lo lote machoni pa Yesu.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy