Sehemu ya Kupata Raha
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mathayo 11:28-30 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.
Nikiongea swala la “mapumziko”,! Ni dhana gani inayotokezea kichwani mwako? Kukaa pwani chini ya nazi kwenye upepo mwanana? Labda ni kujilaza chini ya shuka ukitazamia kulala usiku kucha? Je! Neno “mapumziko” ina maana gani kwako?
Ni jambo jema kila mtu awe anapumzika baada ya kuchoshwa na shughuli zake. Pia, kulala vizuri katika usingizi ni muhimu kwa ajili ya afya ya mtu na ustawi wake. Lakini mtu hawezi kuishi maisha yake yote kwenye likizo na burudani au akilala kitandani tu. Uzima unakuwepo ili mtu aishi maisha yake.
Na hili ndilo lengo alilokuwa nalo Yesu wakati alitwambia habari ya raha, mapumziko yadumuyo anayekusudia kutukirimia nayo.
Mathayo 11:28-30 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.
Hmm. Jitieni nira yangu. Nira, si kiti cha starehe kwenye boti ya kutalii bali ni kifaa cha kazi kinachovalishwa mabegani mwa ng’ombe kwa kusawazisha uzito wa mzigo unaokokotwa.
Ina maana, ni kufungiwa pamoja na Yesu kwenye nira moja, bega kwa bega kupitia upendo wake, hekima yake, mafundisho yake … katikati ya maisha haya, kutimiza yote aliyekuitia uyafanye. Hapo ndipo aliyekusudia uone raha na starehe nafsini mwako.
Usisite kupumzika na kupata muda wa likizo. Lakini baada ya likizo, endelea na maisha yako. Pia … Jitieni nira yake, ujifunze kwake … na utapata raha nafsini mwako.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.