Sisi Sote Tuna Haja Hii
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Warumi 11:5,6 Basi ni vivi hivi wakati huu wa sasa, yako mabaki waliochaguliwa kwa neema. Lakini ikiwa ni kwa neema, haiwi kwa matendo tena, au hapo neema isingekuwa neema.
Mara kwa mara, sisi sote tunajikuta katika hali ya kuhitaji kutendewa mema na kufadhiliwa na watu wengine ili tuweze kustahimili majaribu ambayo tusingeyapitia peke yetu. Ndivyo tulivyo.
Je! Ni lini uliwahi kuhitaji kutendewa hivyo na mtu mwingine? Je! Unakumbuka jinsi ulivyokatishwa tamaa katikati ya changamoto uliyokabiliana nayo?
Ndipo mtu aliyekuonekania akitamka neno la faraja, au labda alikusaidia na kukidhi hitaji uliokuwa nalo na kukuokoa. Mafuriko ya shukrani uliyoisikia wakati ule ni kitu ambacho kuisahau.
Alichokifanya kwa kukuonekania hata kama hukustahili kinaitwa neema. Zaidi ya mambo yote yanayotupata yasiyo ya kawaida, ni wazi kwamba sisi sote tunahitaji neema isiyo ya kawaida.
Kwa sababu ya makosa yote tuliyoyafanya maishani, tusingeweza kamwe kujistahilisha tena machoni pa Mungu hata tukisema nini au kutenda nini. Kila mmoja wetu amepungukiwa na utukufu wake. Kila mmoja wetu anastahili kulipa gharama. Lakini hata hivi …
Warumi 11:5,6 Basi ni vivi hivi wakati huu wa sasa, yako mabaki waliochaguliwa kwa neema. Lakini ikiwa ni kwa neema, haiwi kwa matendo tena, au hapo neema isingekuwa neema.
Umwamini Yesu na unaokolewa na kitu kimoja, kitu kimoja tu. Ni neema ya Mungu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.