... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Siyo Njia Rahisi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mwanzo 3:16,17 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako.

Listen to the radio broadcast of

Siyo Njia Rahisi


Download audio file

Sijui kama utaniruhusu nikikuulize swali sasa hivi? Familia yako inaendeleaje?  Je! Mahusiano ya kifamilia yana kina gani?  Yana nguvu kiasi gani?  Kwasababu kusema ukweli, kuishi kifamilia katika ulimwengu huu tunaoishi, ulimwengu unaoenda kasi ukivurugwa pia na teknolojia ya kisasa, si jambo rahisi.

Tulipokwenda likizo hivi karibuni, tulikutana na mume na mke wazuri sana ambao ilionekana kwamba walifanikisha mambo yao yote vizuri – walikuwa wamestafu, walikuwa na nyumba nzuri sana kwenye uwanja mkubwa nje ya mji, ndoa yao ilikuwa imara, yaani kila kitu.

Lakini huko nyuma ya mwonekano wao mzuri wa maisha bora, kulikuwa ishu nyingi ngumu iliyohusu watoto wao waliokuwa watu wazima sasa.  Hayo yalinifanya kugundua mara tena kwamba hakuna familia iliyokamilika.  Na kuna sababu ina kuwa hivi:

Mwanzo 3:16,17  Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako.

Tunaishi katika dunia iliyolaaniwa, ulimwengu wa dhambi, Ulimwengu unaotubana, Una watu wenye mapungufu. Kwa hiyo, usifikiri ni familia yako tu.Kila familia ina ishu zake.  Kila familia ina matatizo. Lakini kumbuka hili, Mungu anapenda kila familia, anapenda familia yako … kupita maelezo.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy