... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Taabu Nyingi Sana

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Nyakati 30:9 Kwa kuwa mkimrudia BWANA, ndugu zenu na watoto wenu watahurumiwa machoni pa hao waliowachukua mateka, nao watairudia nchi hii; kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye mwenye neema, na mwenye rehema, wala hatawageuzia mbali uso wake, mkimrudia.

Listen to the radio broadcast of

Taabu Nyingi Sana


Download audio file

Unajua kinachonigusa zaidi katika zamani hizi tumamoishi?  Ni kwamba watu wengi sana wanaishi maisha duni, yenye taabu kiasi cha kustaajabisha.  Je!  Kwa nini watu wengi hivi wanapata mateso hayo yote?

Unajua kinachonifanya nisikitike hivi?  Hapa kwetu kwenye huduma yetu ya Ukristo tuna tovuti kwa ajili ya maombezi – PowerfulPrayer.org (Maombi yenye Nguvu) – ambapo watu maelfu duniani kote wanaturushia mahitaji yao ya kuombewa ili jeshi la watu wa maombi liweze kuwaombea.

Na mimi pia ninajaribu kuombea baadhi yao.  Lakini mahitaji ni makubwa, na mazingira ya wengi yanatisha mno mpaka moyo wangu unataka kuvunjika kabisa.

Sasa ebu fikiria jamani, ukizingatia maombi na dua ma-miliyoni hata ma-biliyoni yanayopanda kila siku mbele zake Mungu kila siku, lazima moyo wake uumie sana kwa ajili yetu, tukiwemo wewe na mimi.  Taabu hii yote ni matokeo ya dhambi ya mwanadamu – hata dhambi zako na zangu.

Lakini hata kama dhambi zetu zimesababisha maumivu hayo yote kutuangukia, na kwa sababu ya unyonge wetu, Mungu anayo ya kutwambia siku ya leo.

2 Nyakati 30:9  Kwa kuwa mkimrudia BWANA, ndugu zenu na watoto wenu watahurumiwa machoni pa hao waliowachukua mateka, nao watairudia nchi hii; kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye mwenye neema, na mwenye rehema, wala hatawageuzia mbali uso wake, mkimrudia.

Popote ulipo, haijalishi umepotea kwa umbali gani, umrudie Bwana.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy