Tenda Yanayowezekana
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Ezra 10:4,5 Inuka; maana shughuli hii yakuhusu wewe; na sisi tu pamoja nawe; uwe na moyo mkuu, ukaitende. Ndipo Ezra akaondoka, akawaapisha wakuu wa makuhani, na Walawi, na Israeli wote, ya kwamba watafanya kama hayo. Basi wakaapa.
Wakati mambo hayaendi kama ulivyotazamia, wakati unakumbana na upinzani, wakati unaumia, wakati una hofu, wakati unafadhaika, sehemu zote za nafsi yako zinakupigia kelele – simama, acha, inatosha!
Unajua kwa nini ninafahamu hali hiyo? Ni kwa sababu nimeshaipitia, mara nyingi tu – katika maisha yangu, pia katika huduma yetu ya Ukristo, ambapo nimepashughulikia zaidi ya miaka ishirini. Mara nyingine, mtu anataka kusimamisha gari lake pembeni ya barabara, avute pumzi kidogo hadi bumbuazi imutoke, halafu ageuze na kurudi nyumbani.
Ezra, nabii katika Agano la kale, alikuwa na kazi inayotisha mno. Waisraeli walikuwa wamesharudi katika Nchi ya Ahadi baada ya kuishi mateka Babeli miaka sabini. Mji wa Yerusalemu bado ulihitaji kujengwa na kukarabatiwa, na hata watu walihitaji ukarabati kwa sababu walikuwa wameshaharibiwa na matendo yao maovu.
Jamani! Hali hiyo ingemkatisha tamaa na kusababisha aache kazi na kurudi nyumbani tu. Lakini Ezra alikuwa kiongozi aliyeteuliwa na Mungu atimize kazi hiyo kubwa. Kwa hiyo wananchi walimwambia hivi:
Ezra 10:4,5 Inuka; maana shughuli hii yakuhusu wewe; na sisi tu pamoja nawe; uwe na moyo mkuu, ukaitende. Ndipo Ezra akaondoka, akawaapisha wakuu wa makuhani, na Walawi, na Israeli wote, ya kwamba watafanya kama hayo. Basi wakaapa.
Sikiliza! Inabidi siku zingine kujifanya jasiri, kuinuka tu, kutoka nje, na kuanza, hatua kwa hatua, kuajibika na kutenda yale Mungu amekuitia uyafanye. Najua labda hautapenda kuyasikia lakini ni kweli.
Inuka Ezra; maana shughuli hii yakuhusu wewe.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.