... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Tiba Kali Kulizo Zote

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 6:27-31 Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi, wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi. Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang’anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu. Mpe kila akuombaye, na akunyang’anyaye vitu vyako, usitake akurudishie. Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo.

Listen to the radio broadcast of

Tiba Kali Kulizo Zote

Download audio file

Chuki ilianzia tangu mwanzo kabisa.  Ilianza wakati mwana wa Adamu na Hawa aitwaye Kaini aliua mdogo wake Habili na tangu pale binadamu wameendelea kuwa na kinyongo hadi leo na bado chuki inaendela kuangamiza watu kwa wingi.

Angali Mashariki ya Kati; angalia pia vita vilivyopo maeneo mengi kwenye bara linalopendeza la Afrika, bara lenye rasilimali nyingi mno.  Tazama tena chuki ya ukabila sehemu nyingi duniani.  Kejeli imesambaza uchungu pande zote za siasa, ndoa zimesambalatika na kuharibu maisha ya watoto.

Laiti tungeweza kufuta chuki kutoka kwenye uso wa nchi.  Labda dunia ingekuwa bora sana wakati huu.  Ndiyo maana Yesu aliwaambia watu wa kawaida kama wewe na mimi, maneno yafuatayo:

Luka 6:27-31  Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi, wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi.  Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang’anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu.  Mpe kila akuombaye, na akunyang’anyaye vitu vyako, usitake akurudishie.  Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo.

Hayo ndiyo tiba kali pekee inayoweza kukumbana na chuki katika historia yote ya binadamu:  yaani kufanya kinyume kabisa na mwitikio wa asili dhidi ya chuki.

Napenda sana alichoandika Mmarekani aitwaye Brene Brown, aliye msomi akiwa pia afisa ustawi wa jamii:  Ni vigumu kumchukia mtu uliyemsogelea.  Umsogelee. Tamka ukweli … uwe na adabu.  Shika mikono ya wageni.  Mgongo wako uimarike lakini sura yako ilainike.  Uwe na moyo usiotawaliwa na mazoea na mapokeo.

Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.