Tufuate Neno au Tufuate Ulimwengu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Isaya 40:8 Majani yakauka, ua lanyauka; bali neno la Mungu wetu litasimama milele.
Ulimwengu tunaoishi leo; kweli umebadilika sana – kumekuwa na mabadiliko mengi na makubwa kwenye teknolojia, ulimwengu uko kama kijiji sasa hivi, msimamo wa watu na maadili … hata jinsi watu wanvyofanya kazi siku hizi na kutafuta burudani vimebadilika sana.
Miaka ya 1970 hadi 1980 ni miaka mimi nilikuwa sekondari na chuo. Naona si zamani sana. Lakini mtu akitafakari, kumbe 1972 ni mbali kwa kuangalia nyuma kama vile 2072 ilivyo mbali kuifikia.
Juzi niliangalia picha iliyopigwa katika miaka ya 1970. Ilikuwa picha ya barabara kuu ya mji wetu. Yaani gari na basi zilionekana za kizamani sanaaa, yaani watu walivyokuwa wanavaa na mtindo wa nywele zao, ahahahaha, yaani ni kituko.
Picha ile iliniamsha na kunikumbusha namna ambavyo msimamo wetu umebadilika hususani kumhusu Mungu, na yale anayosema katika Neno lake kuhusu mema na mabaya. Kumbe, mfumo wa jamii umeenda mbali sana na ukweli huo usioweza kubadilika. Na nikisema wazi, hata sehemu isiyo ndogo ya kanisa na waamini ndani ya makanisa wamepelekwa mbali. Kwahiyo, labda muda umewadia wa kuamsha watu.
Isaya 40:8 Majani yakauka, ua lanyauka; bali neno la Mungu wetu litasimama milele.
Yale yote niliyokuwa ninakuelezea mwanzoni … ni kama maua na majani. Mitindo, msimamo, maadili, hayo yote huwa yanabadilika-badilika. Teknolojia … yenyewe inaenda kasi, hatujui kitakachotokea ndani ya miaka mingine mitano.
Kwahiyo, usiruhusu mambo unayoyaona, vitu vinavyoshikika, visababishe usahau alichokisema Mungu – kwasababu hata kama majani yanakauka na maua yananyauka, Neno la Mungu litasimama pale pale milele daima.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.