Tumaini Halisi
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Tito 2:13,14 Tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.
Watu wengi wanao mtazamo hasi kabisa. Labda kwa sasa hivi hauko hivi, lakini najua kwamba umewahi kukatishwa tamaa, kama vile mimi. Swali lililopo ni hili, Je! Mtu anaweza kufanya nini ili awe na matumaini?
Mtu anaweza kuishi maisha ya anasa na mafanikio lakini bado anaweza kumezwa na hali ya kukosa tumaini, hali inayomlemaza kabisa. Niliwahi kupitia hali kama hiyo na kwa kweli kidogo ilitaka kuniangamiza.
Kwa hiyo acha niulize hivi, Je! Kwenye kipimo cha kupimia tumaini, kuanzia sifuri hadi kumi, wewe uko wapi ukitazamia ziku zilizo mbeleni? Wakati bado unatafakari swali langu, acha nilete hoja hii ingine ili nijue unafikiri nini.
Jinsi mtu anaamua kutenda mema siku baada ya siku dhidi ya tabia mbaya ambayo ingemwangusha, ndiyo inayoweza kusababisha awe na matumaini au la. Wewe unaonaje?
Tito 2:13,14 Tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.
Kwangu mimi, mambo yalianza kubadilika siku ile Yesu aliniyonionekania wakati nilikuwa nimeshakatishwa tamaa, wakati nilimwitikia kwa imani. Lakini sikubadilishwa moja kwa moja kutoka sifuri hadi kumi, h. Ilikuwa hatua kwa hatua akiniongoza siku baada ya siku, niweze kuchagua mema kuliko mabaya. Na bado ninaendelea na safari hiyo. Wewe, vipi?
Rafiki yangu, weka tumaini lako kwake Yesu. Alikufa ili akuweke huru na uovu wote. Acha akusafishe na kukuongoza kwenye hali ya kupenda kutenda mema daima.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.