Tumaini la Utukufu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wakolosai 1:27 Ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukutu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu.
Katika ulimwengu huu ambamo dhana ya kweli inazidi kubadilishwa kuwa ovu na kubadilishwa kuwa kama silaha ya kuangamiza maisha ya watu, wengi wetu wanaanza kuogopa na kuacha kutafuta kujua ukweli uko wapi. Ni kwa sababu inazidi kuwa ngumu kujua kweli kwa uhakika.
Jua ya kwamba mambo yatazidi kuharibika. Kuna akili iliyoundwa na binadamu ndani ya mitambo ambayo inaweza kuleta mafao mengi kwa jamii, lakini watu wabaya na wao pia wataweza kuitumia kwa kufuta dhana zote zinazohusu kweli. Mfano – watatengeneza video feki –watamfanya mtu kutamka maneno ambayo kamwe hakuwahi kuyasema – na hii ni mwanzo tu wa kuigiza mambo ya uongo na vitendo visivyo vya kweli kwa kusingizia watu wasio na hatia.
Lakini udanganyifu huo si jambo jipya, umekuja taratibu taratibu. Zamani, katika “vyombo vya habari”, waandishi na watangazaji walijaribu kutoa habari kama ilivyotokea. Lakini sasa vipindi vya “habari” vimekuwa muda wa maoni tu, maoni ya upande mmoja hadi ni vigumu kupata chombo cha habari ambacho kinatoa habari tu bila kuwa na uelekeo fulani au agenda ya chini-chini.
Lakini kuna kweli moja – yenye utukufu mkubwa – ambayo haibadiliki, ya kutegemea kabisa.
Wakolosai 1:27 Ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukutu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu.
Sasa ukimwamini, siri ya kweli hiyo itatimia ndani yako. Ukimwishia yeye, atakuwa anaishi ndani yako.
Kristo peke yake ni tumaini lako la utukufu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.