... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ubatizo wa Roho Mtakatifu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mariko 1:7,8 Akahubiri akisema, Yuaja nyuma yangu aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuinama na kuilegeza gidamu ya viatu vyake. Mimi niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.

Listen to the radio broadcast of

Ubatizo wa Roho Mtakatifu


Download audio file

Je!, Umewahi kujiuliza Ubatizo una maana gani?  Ni zoezi lisilo la kawaida; lakini limetumika karne nyingi – kwanza katika dini ya Wayahudi; baadaye katika Ukristo.  Hata Yesu alibatizwa.

Tuanze mara moja.  Jana tulikutana na Yohana Mtatizaji aliyekuja kumtengenezea Yesu njia kwa kuwatangazia watu wabatizwe; ili waonyeshe kwamba wanataka kubadilisha maisha yao; kuachana na dhambi zilizozinga nafsi zao kwa nguvu.

Hili ni jambo jema – watu wote kutoka Uyahudi kote na Yerusalemu pia walienda kumuona, jamaa huyu aliyeishi nyikani ili aweze kubatizwa.  Kwa kufanya hivyo, Yohana alikuwa anaandaa njia ya Bwana, kufungua mioyo ya watu kwa kupitia zoezi hili la kuoshwa.

Lakini ndugu, niulize, Je!, Umewahi kujaribu kujibadilisha; kupambana na tabia mbaya zilizomo kwenye kiini cha moyo wako, tabia zinazonyonya uhai wako?  imeshindikana, si kweli?  Kwa hiyo …

Mariko 1:7,8  Akahubiri akisema, Yuaja nyuma yangu aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuinama na kuilegeza gidamu ya viatu vyake.  Mimi niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.

Hapa, anaongea habari ya Yesu – ambaye kwa baadaye alikuwa na mengi ya kusema kuhusu kuzamishwa au kubatizwa na kubadilishwa kutokana na uwezo wa Roho Mtakatifu.

Kama umewahi kupambana na dhambi na kushindwa (na ni yupi ambaye hajashindwa?) basi ujue yafuatayo:  Si lazima upambane peke yako.  Kwa sababu; ameshakuja mmoja ili akubatize na Roho wake Mtakatifu.  Ni Yesu.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy