Uende Kasi au Uende Mbali
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 27:17 Chuma hunoa chuma; ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake.
Kazi ya pamoja inasifiwa kote duniani– kwenye kampuni zinazopata mafanikio makubwa, kwenye timu za michezo, kwenye makanisa, ndani ya familia. Ni dhana zuri sana, lakini kuna wengine tuko nao pamoja lakini wanasumbua sana!
Shida iliyopo katika swala la kufanya kazi ya pamoja ni kwamba, sisi sote tuna mitazamo tofauti-tofauti. Sote tunaweza kuangalia ishu fulani lakini tukaitafsiri kwa njia tofauti kabisa.
Halafu kama umeshaona, kila mtu anataka wengine waione kwa mtazamo wake. Kila mtu anataka suluhisho lake lichukuliwe nah ii ni kwasababu anaona yake tu ndio sahihi. utasikia“fanya kama ninavyotaka, la sivyo, mi naondoka zangu!” Sasa kama kila mmoja atasema hivi, hapo ni lazima mgogoro utokee.
Nakumbuka wakati nilipokuwa naongea na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni moja kubwa. Pale nilipogusia habari za idara yake ya menijementi, alicheka sana na kusema, “idara yangu ya menijementi ni kundi la machifu wanaogombana tu siku zote!”
Lakini kama unataka kupiga hatua, lazima uwe na timu, si kweli!?, Kama msemo huu unavyosema: Ukitaka kwenda kasi, basi nenda peke yako. Lakini kama unataka kufika mbali, nenda na wenzako, Hii ni kweli kabisa!
Sasa mtu atafanyaje wakati kila mmoja ana mtazamo tofauti?
Zaburi 27:17 Chuma hunoa chuma; ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake.
Ni kawaida mtu kutaka mawazo yake na utatuzi wake vikubaliwe tu. Lakini badala ya kugonganisha mipango, ni bora tutumie mitazamo yetu tofauti kwakusudi la kunoana. Tukifanya hivyo, ni ajabu kuona jinsi Mungu anaweza kufanya kazi kabisa kupitia kundi lako na kufikia lengo bora. Yaani Lengo la Mungu.
Chuma hunoa chuma; ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.