... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Uepuke Mtego Huu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mithali 29:25 Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; bali amtumainiye BWANA atakuwa salama.

Listen to the radio broadcast of

Uepuke Mtego Huu


Download audio file

Bila shaka umewahi kuwa na hofu maishani mwako. Na mimi pia!  Na kwa kweli, ni mwitikio wa asili uliowekwa ndani yetu kwa usalama wetu. Lakini mtu akiendelea kuishi katika woga muda mrefu, anaweza kuelekezwa pabaya kabisa.

Katika maisha yangu nimejikuta katika ajali ya gari mara mbili na ninakumbuka vizuri namna adrenali yangu ilivyoinuka na kuanza kutawaliwa na hofu kubwa.  Mwitikio kama huo ni mzuri – kwa sababu unamwezesha mtu kuamua haraka na kuwa na nguvu zinazotosha kwa kujihami au kukimbia. 

Lakini hofu ikikawia, na mtu akiendelea kuwa na mashaka makubwa, hasa kwa swala la ki-msingi katika maisha, anaweza kufanya maamuzi mabaya sana, yanayoweza kumwathiri. Kwahiyo tuulize.  Je!, Tufanyeje pale tunapokwama kwenye hofu?. Mtu atapambanaje na hali kama hiyo? 

Mithali 29:25  Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; bali amtumainiye BWANA atakuwa salama. 

Ni kweli kabisa.  Kuogopa ni mtego; ni hatari kuendelea kuishi katika hofu.  Lakini amtumainiye BWANA atakuwa salama.  

Je!, Hii ina maana kwamba hatutapata shida tena?  Kwamba hatuwezi kuumia tena?  Kwamba hatutapoteza kitu?  Kwamba hatutakufa?  Hapana!  Lakini hata ukifikia muda wa kufa, kama unamwamini Yesu, utakuwa salama mikononi mwake.  

Na njia ya pekee ninayoijua mimi ya kuishia mstari huo na kupata amani ya Mungu katika vipindi vinavyotisha na kufungua Biblia yangu na kumruhusu Roho Mtakatifu aandike ahadi za Mungu moyoni mwangu; pamoja na kumwomba anipe amani yake ipitayo ufahamu wetu.

Na Mungu hajaniangusha, hata siku moja, hata ikiwa katika vipindi vinavyotisha kweli kweli. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy