... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ufalme wa Mungu Umefanana na …

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 13:31,32 Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya haradali, aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake; nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hata nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake.

Listen to the radio broadcast of

Ufalme wa Mungu Umefanana na …


Download audio file

Hili ni tatizo ambalo watu wengi wanakabiliana nalo:  Mtu anataka kuwa na imani, yaani awe na sehemu ya kiroho maishani … ila, katikati ya pirika za kila siku, sehemu hiyo inaonekana kuwa finyu, bila maana sana … ikizidiwa na kelele zilizopo pande zote.

Sijui kama umeshaona hayo?  Mimi nimeyashuhudia kabisa kwa sababu najua kwamba maisha ni magumu, ni kujitahidi tu. 

Mathayo 13:31,32  Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya haradali, aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake; nayo ni  ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hata nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake.

Ujue kwamba wasikilizaji wake walielewa vizuri dhana ya “ufalme”, yaani utawala na madaraka ya mfalme fulani.  Hapo awali walikuwa na wafalme wao Waisraeli, lakini wakati wa Yesu, taifa ilikuwa chini ya utawala wa kikatili wa Kaisari huko Rumi.  Sasa … Yesu alitaka kusema nini hapo?

Ina maana, wakati mtu anapanda punje ya haradali ya imani moyoni mwake (mbegu ndogo kuliko zote) itakuwa haraka kama ilivyo asili ya miti ya haradali na kuwa mti mkubwa sana; yaani imani ile hatimaye itakuwa jambo linalotawala maisha yako.  Imani kubwa hadi watu wengine wataweza kuja kupumzika ndani yako kama vile ndege wanavyotua ndani ya mti ule.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy